Tangu enzi za zama, kabla kuzaliwa baba na mama,
Hakuna mtu aliyezama, kuelekea kwa mama pima,
Babu alitoka huku akikwama, aghalabu kuhitaji rukwama,
Nyumbani alifika salama,
kupunguzia nyanya gharama.
Vivyo hivo walifanya, walofuata baadae,
Kila siku baba alipenya, asiwaache wanae,
Mama naye kutukanya, pombe heri ikae,
Hayo yote yalinifinya, Athumani niokolee.
Kwa sababu wakati ule, haikuwa shida kwa kinywa,
Nakumbuka tembo ile, ilihitaji kufinywa,
Ili ifike kiwango kile, kisohitaji kukanywa.
Kumbuka hivi juzi, ilivyochukua roho kasi,
Mama atokwa na chozi, mtoto kajaa kamasi,
Baba yetu kafa ja mwizi, kalazwa kama mjusi.
Hata hamwoni haya, kunambia nyasi itamea,
Nawe ulozoea kaya, nami basi nakukemea,
Chunga usikanyage nyaya, nao ukauke mmea.
No comments:
Post a Comment